Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

..

Saturday, December 15, 2012

NJIA YA KUONDOA CHUNUSI NA MABAKA USONI

 Njia ya kuondoa Chunusi na mabaka usoni
Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama vivimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.
Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa . Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe Karibu asilimia 85 ya  vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na  zaidi ya  asilimia 20 ya wanawake  wenye umri wa zaidi ya miaka  ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe.
Vipele vinaweza kuwa vidogo  au vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali hii hutokea pale ambapo seli za ngozi zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.Ngozi mpya hutengenezwa kirahisi tu  mahali palipokuwa na chunusi hali hii husababisha mlingano usiosahihi wa  ngozi na hutoa kidonda ambacho baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega na mgongoni.
Chanzo cha Chunusi
Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;
Umri
Kama nilivyosema( hormone)vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubalehe.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa  nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
Vipodozi
Baadhi ya vipodozi vya usoni(Make-up) za kina dada na Marashi(spray) za nywele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
Chakula
Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufanya chunusi kuwa nyingi zaidi.Hasa vyakula vyenye mafuta.
Dawa
Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na makusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.
Magonjwa
Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana
Mazingira
Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye  mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekano wa kupata chunusi.
Jinsia
Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.
Familia
Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia  wa familia kadhaa kuliko nyingine.
Homoni
Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
Usafi wa mwili
Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au vipele  husababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwilini au kutooga huongeza uwezekano wa kupata chunusi
Mawazo(Stress)
Mtu anapokuwa na mawazo mengi vikemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huweza kuchangia au kusababisha chunusi
Dalili za Chunusi
Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.Wakati mwingine huweza kujitokeza kama baka dogo.
Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi sana Daktari kuzigundua,japokuwa katika familia zetu ni mara chache sana mtu akaenda kumwona daktari  au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya chunusi.Pale vinapotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya  zaidi.Hata hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu, chakula,ngozi,dawa unazotumia na vitu vingine vinavyoweza.kuchangia mtu kupata chunusi
Matibabu
Matibabu ya chunusi yanajumuisha  kupunguza utoaji wa (sebamu ),kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingi au ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama nilivyokwishakueleza katika makala iliyopita.
Dawa za kupaka
Kuna dawa za kupaka ambazo hupakwa katika eneo la ngozi lililoathirika kwa chunusi.Dawa hizi hupatikana kama cream,losheni,jel .Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu.
Dawa nyingine ni zile zinazolainisha nta  na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi
Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi  na sabuni ya kawaida na kukausha kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.
.
Matibabu mbadala
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu na kuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.
Watu wenye chunusi wanashauriwa  kula mlo kamili wenye vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi,matunda , mboga za majani,vitamin B. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa,tumbaku,sukari,vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi.
Mambo ya kuzingatia ili usipate Chunusi
Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
·      Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi  kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu chochote kigumu.
·      Tumia  Vipodozi au vilainisha ngozi visivyo na mafuta  ya mgando
·       Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
·      Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
·      Usibinye au kutoboa  vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.
·      Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
·      Punguza mawazo

Kumbuka kuwa chunusi haziwezi kutibika kabisa   iwapo matibabu yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona  na unapokuwa unatumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.

Ukitaka kuondoa chunusi usoni na kusafisha uso usiwe na madoa kwa nija ya kiasili, njia zifuatazo zaweza sana kukusaidia.Tafuta ukwaju loweka katika maji ukishalainika changanya na asali, paka usoni.Ni dawa nzuri sana na utaona ngozi yako inabadilika kwa kipindi kifupi.
Kama utashindwa kupata vitu hivyo tafuta sabuni pamoja na krimu yenye mchanganyiko wa asali na ukwaju,lakini nadhani asali na ukwaju kama utaenda sokoni ni rahisi kupata.Pia ni vema ukitumia losheni yenye mchanganyiko wa asali au ukwaju.Kwa matibabu zaidi piga simu namba0754201666,kumbuka kuwa ni kwa ajili ya matibabu ya ngozi na chunusi za aina yoyote.
0 comments:

Post a Comment